Shirika la Habari la Hawza, linachapisha riwaya ifuatayo kutoka katika kitabu “Mustadrak al-Wasā’il.”
Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema:
صَلاَةُ اَلرَّجُلِ فِي جَمَاعَةٍ خَيْرٌ مِنْ صَلاَتِهِ فِي بَيْتِهِ أَرْبَعِينَ سَنَةً قِيلَ يَا رَسُولَ اَللَّهِ صَلاَةُ يَوْمٍ؟ فَقَالَ: صَلاَةٌ وَاحِدَةٌ، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّی اللَّهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ: إِذَا كَانَ اَلْعَبْدُ خَلْفَ اَلْإِمَامِ كَتَبَ اَللَّهُ لَهُ مِائَةَ أَلْفِ أَلْفٍ وَعِشْرِينَ دَرَجَةً
“Swala ya mtu anayeswali jamaa ni bora kuliko swala yake anayoiswali nyumbani kwake kwa muda wa miaka arobaini.” Pakasemwa: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je, unamaanisha swala ya siku moja?” Akasema: “Swala moja.”
Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Mja anapokuwa nyuma ya Imamu, Mwenyezi Mungu humwandikia daraja laki moja na ishirini.”
Chanzo: Mustadrak al-Wasā’il wa Mustanbat al-Masā’il, Juzuu ya 6, uk. 446.
Maoni yako